FURSA 13 MUHIMU ZA UWEKEZAJI KWA WAJASILIAMALI - KAZI MUBASHARA

Header Ads

FURSA 13 MUHIMU ZA UWEKEZAJI KWA WAJASILIAMALI

 Zifuatazo ni baadhi ya fursa  zilizopo Tanzania ambazo wajasiliamali wanaweza kuzitumia kupanua biashara zao
01. NGOZI

Related image
Sekta ya ngozi inatoa fursa kubwa ya kuwekeza katika uzalishaji. Tanzania huzalisha takribani vipande milioni 2.6 vya ngozi ghafi kwa mwaka, wakati ambapo inayochakatwa nchini ni asilimia 10 na sehemu kubwa inasafirishwa nje ya nchi kama mali ghafi.
 Fursa katika eneo hili zipo ili kuwekeza katika uzalishaji wa kisasa katika sekta ya ngozi na mazao yake kama viatu, mikoba, mikanda, na bidhaa nyingine za ngozi.
 02. VIBALI NA LESENI ZA UKANDA MAALUM WA KIUCHUMI (SEZ)
Image result for LESENI YA BIASHARA PICS
 
 LESENI YA MWEKEZAJI
Hii inatolewa kwa mwekezaji anayetaka kuwekeza katika miundo mbinu kama vile ujenzi wa majengo ya viwanda na maghala, ujenzi wa barabra za ndani, usawazishaji mazingira na ujenzi wa uzio pamoja na utoaji huduma za jamii kama vile nishati, maji, maji taka na mawasiliano.

Leseni ya Uendeshaji Hii hutolewa kwa mwekezaji anayeendesha shughuli za uzalishaji katika ukanda huu malum (EPZ). Uendeshaji unaweza kuwa katika uzalishaji au uchakataji shughuli za biashara kama vile mwendeshaji kupunguza taka za malighafi, kuandaa vifungashio, uandikaji wa maandishi ya juu ya vifungashio, biashara, huduma zinazohusiana na biashara ya nje ya nchi pamoja na udalali, masuala ya habari na ushauri wa kitaalamu na huduma za matengenezo ya vitu mbalimbali.
Leseni ya Utoaji Huduma Leseni hii hutolewa kwa wawekezaji wanaotaka kutoa huduma kwa kanda hizi maalum za kiuchumi. Wanaitwa watoa huduma na wanapewa leseni ya utoaji huduma kulingana na huduma watakazotoa kuanzia huduma za benki, bima, na Teknolojia ya habari na mawasiliano.
Taratibu za Kupata Leseni za Ukanda Maalum wa Uchumi (SEZ)
  • Mwekezaji anatakiwa kupeleka pendekezo la mradi katika ofisi za ukanda huu maalum wa kiuchumi (EPZA), kwa kujaza fomu za maombi na kukusanya mpango wa mradi na fomu ya maombi vyote kwa pamoja na ada isiyorudishwa kiasi cha dola za Marekani 250.
  • EPZA hutathmini mapendekezo ya mradi na kutoa barua ya maidhinisho kwa mwekezaji na kwa kawaida huchukua kati ya siku mbili mpaka tatu.
  • Mwekezaji anapata usajili wa kampuni ndani SEZ, halafu anapatiwa eneo/ardhi na kibali cha mazingira (pale kitakapohitajika).
  • Kwa maendeleo ya ukanda huu, EPZA huwezesha kupatikana kwa ardhi kutoka kwa Waziri wa Biashara na Viwanda.
  • Mwekezaji atatakiwa kulipa ada husika za leseni na hupewa leseni ya ukanda huu. Ada ya mwaka kwa mwenedelezaji wa SEZ ni dola za Marekani 5,000 wakati ada ya mtumiaji wa SEZ ni dola za Marekani 1,000 ambayo hulipwa ya kipindi cha miaka mitatu.
Baada ya taratibu hizo mwekezaji anaruhusiwa kuanza uendeshaji wa shughuli zake za kibiashara alizozikusudia.Taratibu za Kupata Leseni za Ukanda Maalum wa Uchumi (SEZ)Mwekezaji anatakiwa kuulizia katika ofisi za ukanda huu EPZA kuhusu fursa ili kuthibitisha taratibu za uwekezaji, masharti ya uhakiki na uwezekano wa eneo la kiwanda au eneo la huduma
Kanuni zinazoongoza shughuli za EPZ na SEZ
Sheria ya Kanda Maalum ya Usafirishaji wa Bidhaa Nje (Export Processing Zone Act), 2012 Hii ni sheria inayopelekea uanzishaji, uendelezaji na uendeshaji wa Kanda hii maalum ya kiuchumi (EPZ) ili kuanzisha biashara za kimataifa kwa kukuza biashara ya nje na masuala yanayoendana na biashara katika ukanda huo. Sheria inaeleza kuhusu vivutio vinavyotolewa kwa wafanyabiashara katika kanda. Inatoa mamlaka na nguvu ya lutoa leseni na vibali Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uchumi (EPZA), na inaeleza masuala yote yanayoendana na biashara na shughuli zote katika ukanda huu (EPZ) (soma sheria yote).
Sheria ya Kanda Maalum za Kiuchumi (The Special Economic Zones Act (revised) ), 2012 Sheria hii ilipitishwa kwa ajili ya maendeleo na uendeshaji wa kanda maalum za uchumi ili kuanzisha mazingira ya kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ili kuwezesha kupanua ajira, kupata ukuaji uchumi na kutoa fursa zinazoambatana nayo (soma sheria yote).
Kanuni za Ukanda Maalum wa Kiuchumi (The Special Economic Zones Regulations), 2012 Hizi ni kanuni maalumu zinzotoa maelekezo ya namna ya kuendesha SEZ. Kanuni zinaeleza kuhusu taratibu mbali mbali na masharti anayotakiwa mtu kujihusisha na shughuli za biashara za SEZ.
Pia zinatoa taarifa kwa makosa na faini kwa atakayeendesha shughuli ndani ya kanda bila leseni maalumu (soma kanuni zote).

03. UKANDA MAALUM WA UUZAJI BIDHAA NJE YA NCHI/ EXPORT 
Image result for EXPORT TRADE PICS
Mpango maalum kwa ajili uanzishaji wa uwekezaji unaolenga katika mauzo ya bidhaa nje ya nchi kwa ili ya kuanzisha ushindani wa kimataifa ili kuwezesha uchumi utakaojikita katika kusafirisha bidhaa zilizozalishwa Tanzania.
Kanda Maalum za Uchumi Mpango huu una madhumuni ya kuwezesha ukuaji wa haraka wa uchumi, kukuza mapato ya nje, kutengeneza ajira na kuvutia wawekezaji binafsi kwa njia ya Uwekezaji wa Nje wa Moja kwa Moja (FDI) na Uwekezaji wa Ndani wa Moja kwa Moja (DDI) katika sekta zote za uzalishaji na utoaji huduma.
Maeneo yenye Vipaumbele
Uendelezaji Miundombinu: Kwa kutumia mpango wa Kanda Maalum ya Uchumi (SEZ), mwekezaji anaweza akaanzisha maeneo ya viwanda na biashara katika Kanda Maalum ya Uchumi (SEZ). Uwekezaji kwa upande wa miundombinu unaweza kufanyika kupitia ujenzi wa barabara, huduma za jamii, na masuala ya msaada wa kiutawala na maeneo yanayohusu huduma.
Uzalishaji: Wawekezaji wanaweza kuanzisha shughuli za uzalishaji katika Kanda Mahsusi ya Uchumi kwa kutumia Leseni ya Ukanda Maalum wa Kiuchumi (SEZ) au kwa kutumia Leseni ya Kusafirisha Bidhaa Nje ya Nchi ya mpango huu na kunufaika na faida mbalimbali zinazotokana na mpango huu. Miongoni mwa za fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania ni pamoja na usindikaji wa mazao ya kilimo, vito vya thamani (madini), uchakataji wa ngozi, usindikaji wa samaki, misitu na mazao ya misitu, na viwanda vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na uundaji.
Biashara na Huduma: Wawekezaji wanakaribishwa kuanzisha uendeshaji wa biashara na huduma katika Kanda za Biashara Huria na Bandari Huria ambazo kwa kiasi kikubwa bado fursa hizi hazijatumika.
Utalii: Wawekezaji wanaweza kuwekeza katika maendeleo ya utalii kupitia Kanda Maalumu za Kiuchumi kwa kutumia Leseni ya kanda hiyo. Miradi inaweza kuwa ya hoteli, makumbusho, sehemu za kuburudisha na kilabu za gofu. Sifa za kuwekeza kupitia SEZ: Mwekezaji ye yote ana sifa za kuwekeza chini ya Mpango Maalumu wa Kanda za Uchumi. Mwekezaji sharti atimize vigezo vifuatavyo:
  • Uwekezaji lazima uwe mpya, kwa maana ya usiwe uwekezaji ambao umeshafanyika katika ukanda huu maalum
  • Mapato ya biashara ya usafirishaji bidhaa nje ya nchi isiwe chini ya dola milioni tano kwa mwekezaji mgeni kwa mwaka na yasiwe chini ya dola za Marekani millioni moja kwa wawekezaji wazawa.
  • Lazima muwekezaji ahakikishe Usalama wa mazingira unaojitosheleza
  • Utumiaji wa vifaa vya kisasa katika uchakataji na mitambo mipya
  • Mwekezaji lazima awe katika maeneo yaliyoainishwa katika paki za Kanda Mahsusi za Uchumi (SEZ) kama vile Ukanda maalum wa uwekezaji wa Benjamini William Mkapa uliopo Mabibo, Dar es salaam.
   04. NGUO NA MAVAZI
Image result for CLOTHES INDUSTRY PICS
Kuna fursa za kuanzisha viwanda vya nguo jumuishi pamoja na viwanda vya kusindika na kuchakata pamba. Fursa hii nchini Tanzania ipo kulingana na ukweli kwamba kuna uzalishaji mkubwa wa pamba unaopelekea zao hili kukosa soko muda mwingine. Hii ikitiliwa maanani na wajasiriamali aidha mmoja au vikundi inaweza kuleta tija katika kukuza uchumi wa wajasiriamali.

05. KUSINDIKA MATUNDA/ MBOGA
 Image result for USINDIKAJI WA  MATUNDA PICS
Tanzania ina utajiri mkubwa wa aina nyingi za matunda na mbogamboga. Ni chini ya asilimia 10 tu ya matunda na mboga zote zinazozalishwa zinasindikwa. Maeneo yenye ardhi inayokubali kilimo cha matunda ni mikoa kama ni Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya, Mwanza na Kagera.

05. UZALISHAJI 
Image result for UWEKEZAJI PICS
Sekta ya uzalishaji iko katika hatua changa ikiwa na maeneo machache yanayotumika ambapo kwa kiasi kikubwa inatawaliwa na mazao ya kilimo yanayosafirishwa yakiwa hayajachakatwa. Fursa zilizopo katika sekta hii ni kupitia uzalishaji kwa ajili ya watumiaji wa kawaida bidhaa kama vyakula, vinywaji, nguo, tumbaku, mbao, mazao ya mbao, mazao ya mipira, chuma, na bidhaa za chuma.

06. UTALII
 Image result for UTALII PICS
Zaidi ya asilimia 44 ya ardhi ya Tanzania ina maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wanyamapori na hifadhi za taifa. Kuna hifadhi za taifa 16, maeneo 29 yaliyotengwa kwa wanyamapori, maeneo 40 chini ya udhibiti wa uhifadhi na hifadhi ya maeneo katika mwambao wa bahari. Uwekezaji katika utalii waweza kuwa katika njia ya malazi (mahoteli, kambi za kitalii), huduma za utalii na ufanyaji shughuli zinazoendana na utalii na uwakala katika utalii.

 07. UFUGAJI WA NYUKI
Image result for UFUGAJI WA NYUKI PICS
Fursa zipo kwa ajili ya viwanda na usambazaji wa vifaa vya kutumika katika ufugaji nyuki, kwa mfano, mizinga ya nyuki, vifaa vya kinga, na vifaa vya kurina asali. Upande mwingine kwa uwekezaji katika ufugaji nyuki ni kutengeneza viwanda vya mishumaa, rangi za kung’arishia viatu, rangi kung’arishia mbao, vilainishi na bidhaa za famasia. Pia viwanda vya vifungashio vya asali na viwanda vinginevyo vinavyotumia asali kutengenzea pombe, mvinyo, na waokaji vyakula pia wanaweza kutumia fursa hii.

08. MISITU 
 Image result for MISITU PICS
Serikali inafanya juhudi kubwa katika kukuza sekta binafsi na ushiriki wa jamii katika uendeshaji wa mashamba ya serikali. Serikali ianajaribu kuzishawishi kampuni na watu mmoja mmoja kuwekeza katika ukulima wa miti ya magogo, kupitia ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi. Uanzishwaji wa viwanda unahitajika ili kutumia vizuri mazao ya misitu kuzalisha mbao, aina mbalimbali za mbao, samani na nguzo.

09. UVUVI
Image result for UVUVI PICS
Tanzania ni nchi ya kumi kwenye shughuli za mazao ya uvuvi. Fursa kubwa zinazopatikana katika sekta ya uvuvi nchini Tanzania zipo katika maeneo kama: uvuvi, usindikaji wa samaki, uongezaji wa thamani ya samaki na bidhaa nyingine za samaki; ujenzi wa boti, ujenzi wa bandari za uvuvi, ujenzi wa bandari kavu, utalii unaohusisha utunzanji wa mazingira, utengenezaji wa vifaa vya uvuvi. Eneo jingine muhimu la uwekezaji kwa wajasiriamali kwenye upande wa uvuvi ni ufugaji wa samaki aina ya kamba, ufugaji wa samaki kaa, ufugaji utamaduni lulu, ufugaji wa finfish, ukulima wa mwani, na uzalishaji wa chakula cha samaki.

10. KILIMO CHA BUSTANI
 Image result for BUSTANI PICS
Hii ni fursa nyingine kwa wajasiriamali nchini kupitia kilimo cha mboga mboga, matunda, maua, viungo na mbegu kwa ajili ya kuuza nchini, katika ukanda wa Africa Mashariki na kimataifa. Kuna upatikanaji usio wa uhakika wa mazao yanayokidhi ubora na viwango kiasi cha kuifanya nchi iagize matunda, mboga mboga na viungo mbali mbali kama vile nyanya, vitunguu, vitunguu swaumu, matufaha, zabibu, mapeasi na matunda madogo aina ya strawberry.
Kwa bidhaa za matunda zinazokidhi viwango, mahitaji ni makubwa sana kwa soko la ndani na hata kwa ajili ya kusafirisha, na hata kiasi cha matunda kianchosafirishwa kutoka Tanzania kimeongezeka maradufu.

11. UFUGAJI
Image result for UFUGAJI PICS

Fursa nyingine kwa wajasiriamali wa Tanzania ni katika sekta ya ufugaji. Katika sekta hii kumekuwepo na uongezekaji wa mahitaji ya bidhaa za ufugaji, hususani nyama. Hii inatokana na ongezeko la watu, ukuaji wa miji pamoja na ukuaji wa vipato baina ya watanzania inaongeza mahitaji ya nyama. Kwa makadirio ya matumizi ya nyama kwa kilogramu 12 kwa mwaka kwa mtu mmoja, soko lanyama kwa Tanzania linakadiriwa kufikia mara tatu ya sasa hivi ifikapo mwaka 20130. Mbali ya soko la ndani la nyama, Tanzania pia inasafirisha nyama kwenda nchi jirani na nchi za Mashariki ya Kati.

12. UKULIMA WA MPUNGA
Image result for MPUNGA PIC
Kwa kuzingatia ukuaji wa pato la taifa ni fursa nyingine ya uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania. Wajasiriamali wanashauriwa kutumia pengo lililopo la usambazaji wa mchele ili kuhudumia mahitaji ya soko linalokua kwa kasi nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kutokana ukuaji wa ongezeko la watu maeneo ya mjini nchini Tanzania unaokadiriwa kufikia asilimia 4.7%, inasadikiwa kuwa watu wengi wa daraja la kati kimaisha nchini Tanzania wanapendelea mchele kama chakula kikuu kulinganisha na vyakula vingine, kwa hiyo hali hii inaongeza tija kwa wajasiriamali watakaojishughulisha na ukulima wa mpunga kuwa na uhakika wa soko linalokua kila mwaka.
Vile vile wajasiriamali wa Tanzania wanayo fursa nyingine ya soko la Afrika Mashariki, Soko la muungano wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC), na COMESA, ambako mahitaji ya mchele yanaongezeka kila baada ya muda. Mikoa ambayo kilimo cha mchele kinakubali nchini Tanzania ni kama Morogoro na Mbeya. 

 13. UZALISHAJI WA MIWA
Image result for KILIMO CHA MIWA PICS
Kutokana na ongezeko la watu na ukuaji wa kipato miongoni mwa watanzania, ukuaji wa soko la sukari Tanzania unakadiriwa kufikia asilimia 6% kwa mwaka. Upungufu wa usambazaji wa sukari kwa sasa unakadiriwa kufika tani 300,000.
Takwimu hizi zinategemewa kupanda kwa kasi kwa sababu wazalishaji wa sukari waliopo hawajaongeza uwezo wao wa kuzalisha kulingana na ukuaji wa mahitaji. Mbali na upungufu huo ndani ya Tanzania, upungufu wa sukari kwa soko la Afrika Mashariki unakadiriwa kufikia tani 400,000 kwa mwaka. Kwa kuzingatia hayo uzalishaji wa sukari ni fursa ambayo wajasiriamali kwa ujumla wanatakiwa kuitumia ili kujiongezea kipato. Mikoa kama Kagera na Morogoro ndio mikoa ambayo kilimo cha miwa kinashamiri vizuri.





 


 

No comments:

Powered by Blogger.