Ajira Mpya kwa Walimu wa Sayansi, Lugha na Mafundi Sanifu Mwezi Agosti 2018. - KAZI MUBASHARA

Header Ads

Ajira Mpya kwa Walimu wa Sayansi, Lugha na Mafundi Sanifu Mwezi Agosti 2018.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU WA
MASOMO YA SAYANSI, LUGHA (FASIHI KATIKA KIINGEREZA)
NA FUNDI SANIFU MAABARA KWA SHULE ZA SEKONDARI AGOSTI, 2018
Ofisi ya Rais – TAMISEMI inapenda kuutarifu Umma kuwa, jumla ya
Watumishi 2,160 wamepangiwa vituo vya kazi kwenye Shule
mbalimbali za Sekondari nchini. Watumishi hao ni Walimu wa Masomo
ya Sayansi na Hisabati, Lugha (Fasihi katika Kiingereza) na Fundi
Sanifu Maabara. Waajiriwa hao waliopangiwa vituo vya kazi
wanatakiwa kuripoti katika Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri
zilipo shule walizopangiwa na baadaye kuripoti kwenye Shule
walizopangiwa kuanzia tarehe 23 Agosti, 2018 hadi tarehe 05
Septemba, 2018 wakiwa na mahitaji yafuatayo:
(i) Vyeti halisi vya taaluma vya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita;
(ii) Vyeti halisi vya kitaalaam vya Mafunzo ya Ualimu vya ngazi
husika; na
(iii) Cheti halisi cha kuzaliwa.
Waajiriwa wapya waliopangiwa vituo vya kazi wanaelekezwa kuwa:
Waajiriwa wapya waliopangiwa vituo vya kazi wanaelekezwa kuwa:
i. Waajiriwa wote waripoti kwenye vituo walivyopangiwa na
kwamba vituo vyao vya kazi ni katika Shule za Sekondari
walizopangiwa na sio Makao Makuu ya Halmashauri;
ii. Mwajiriwa ye yote atakayechukua posho ya kujikimu, kisha
asiripoti katika kituo chake cha kazi alichopangiwa, Serikali
atamchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za nchi;
iii. Hakuna Mwajiriwa atakayebadilishiwa kituo alichopangiwa kwa
sababu yoyote ile. Walimu ambao hawataripoti katika vituo vyao
ndani ya muda uliotolewa nafasi zao watapangiwa Walimu wengine
wenye sifa waliokosa nafasi.
Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo Watumishi hao wamepangiwa,
wawapokee kwa kuzingatia taratibu na kanuni zote za utumishi na
baadaye kutoa taarifa ya kuripoti kwa walimu hao. Taarifa ya
Waajiriwa hao zijazwe kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa taarifa
zaWtumishi wa ajira mpya katika Tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI
(Local Government Staff Recruitment System – LGSRS) mara baada ya
Mwajiriwa kuripoti.
Majina ya Walimu waliopangiwa vituo vya kazi yanapatikana katika
tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz.
Imetolewa na
20/08/2018 KATIBU MKUU

No comments:

Powered by Blogger.